Kulingana na Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a) –ABNA– Hassan Sadra’i Aarif, Msimamizi wa tukio la pili la vyombo vya habari la "Nahnu Abna’ Al-Hussein (aa)" aliongea katika hafla ya kufunga tukio hilo, akisema: "Kadri tunavyosaidia Arubaini kuonekana zaidi katika anga za kimataifa, ndivyo tunavyochangia kutimiza ustaarabu wa Kiislamu."
Hassan Sadra’i Aarif aliongeza: "Tunaona juhudi wazi za kuzuia (kususia) habari kuhusu Arubaini, na njia bora ya kuvunja vizingiti hivi vya vyombo vya habari ni kutumia jukwaa la vyombo vya habari. Kwa hivyo, uteuzi (uchaguaji) wa fani za tukio la Nahnu Abna’u Al-Hussein (as) ulitegemea mtazamo huu, na teknolojia ya akili bandia ilizingatiwa katika uteuzi (uchaguaji) huo."
Mkurugenzi wa Shirika la Habari la ABNA aliongeza: "Kwa Msaada wa Wafanyakazi wa ABNA, tumeanzisha upya lugha kumi na mbili katika shirika hili la habari, na tumeona ongezeko la mara kumi na nne katika mitandao ya kijamii ya ABNA, na ongezeko la wazi la uzalishaji wa maudhui."
Alimalizia kwa kusema: "Tuko tayari kuandaa tukio la tatu la Nahnu Abna’ Al-Hussein (as) kwa kushirikiana na taasisi za kitamaduni na kimataifa kwa wigo mpana zaidi."
Your Comment